1. Guest House Details
Q: What types of rooms are available (e.g., single, double, family)?
Our spacious Double Room features:
- A comfortable 5 x 6-foot bed
- A fan for cooling
- A TV for your entertainment
- A private bathroom
- A desk and chair for working on your laptop
- A cozy sofa for relaxing after a long day
The room is designed for both work and relaxation, making it ideal for travelers looking for comfort and convenience.
Q: What facilities are offered (e.g., free breakfast, Wi-Fi, TV)?
- TV: Available in all rooms.
- Breakfast: Freshly prepared and available upon request from the on-site SHIKA Restaurant (not included in the room rate). Guests can also order special meals.
- 24/7 Caretaker: A caretaker is always on-site to assist with any needs during your stay.
- On-Site Bar: Enjoy drinks at the incorporated bar, open until late hours.
- Security: The guest house is secure, located directly opposite the district police station.
Q: Are the rooms air-conditioned?
No, the rooms are not air-conditioned. However, each room includes a fan for cooling. Our location benefits from a temperate climate, ensuring a comfortable stay.
2. Booking and Payment
Q: Can guests book online or through third-party platforms (e.g., Booking.com)?
Online booking is currently unavailable. Guests can book by calling us directly.
Q: What payment methods are accepted?
We accept payments via cash, mobile money, or bank transfer. We are flexible to accommodate your preference.
Q: Is a deposit required for bookings?
No, we do not require a deposit for bookings.
3. Policies
Q: What is the cancellation policy?
Cancellation is easy—just inform the caretaker about your intention to cancel.
Q: What are the check-in and check-out times?
- Check-in: From 11:00 AM
- Check-out: Strictly before 10:00 AM
Q: Are guests allowed to bring pets?
No, pets are not allowed.
4. Location and Accessibility
Q: Where is the guest house located?
Sukuma Guest House is located about 100 km from Mwanza city center in Nyashimo Township, Busega District, Simiyu Region. It is situated along the Mwanza–Musoma highway and near the shores of Lake Victoria.
Q: How can guests reach it (public transport, taxi)?
- By private car
- By public transport: Buses traveling from Mwanza to Bunda, Bariadi, Musoma, Tarime, or Nairobi pass frequently, about every half an hour.
Q: Are there attractions nearby?
Yes, there are exciting attractions nearby:
- Serengeti National Park: The guest house is just 40 km from Lamadi, where you can find the park's entry gate. Serengeti is known for its large herds of wildebeests, gazelles, and zebras, as well as Africa's only remaining vast land-animal migrations. It is a UNESCO World Heritage Site and an international tourist attraction.
- Lake Victoria: Visitors can enjoy local cultural experiences, such as exploring nearby fishing villages or ordering traditional meals at our restaurant.
5. Special Services
Q: Do you offer airport pickup or tours?
No, we do not currently offer airport pickup or tours.
Q: Is there a restaurant or kitchen available for guests?
Yes, Sukuma Guest House includes an on-site pub and restaurant. We offer:
- A variety of drinks
- Delicious local dishes, including traditional Sukuma cuisine
All meals are prepared by Ms. Shikalile, the proprietor of our renowned SHIKA Restaurant. In addition to accommodation, we provide guests with the opportunity to enjoy authentic local flavors.
________________
1. Maelezo ya Nyumba ya Wageni
Swali: Je, kuna aina gani za vyumba (mfano, chumba kimoja, viwili, au vya familia)?
Chumba chetu kikubwa cha Double kina:
- Kitanda chenye urefu wa futi 5 x 6
- Feni kwa ajili ya kupoza
- Televisheni kwa burudani yako
- Bafu ya kibinafsi
- Meza na kiti kwa kazi za laptop
- Sofa ya kustarehe baada ya siku ndefu
Chumba hiki kimeundwa kwa ajili ya kazi na mapumziko, na ni bora kwa wasafiri wanaotafuta faraja na urahisi.
Swali: Huduma gani zinapatikana (mfano, kifungua kinywa, Wi-Fi, TV)?
- Televisheni: Inapatikana katika baadhi ya vyumba.
- Kifungua Kinywa: Kinapikwa upya na kinapatikana kwa maombi kutoka mgahawa wa SHIKA uliopo (sio sehemu ya gharama ya chumba). Wageni wanaweza pia kuagiza chakula maalum.
- Huduma ya 24/7: Msimamizi yupo muda wote kusaidia mahitaji yako wakati wa kukaa kwako.
- Baa ya Ndani: Furahia vinywaji kwenye baa yetu, ambayo iko wazi hadi usiku wa manane.
- Usalama: Nyumba ya wageni ipo salama, na iko moja kwa moja mkabala na kituo cha polisi cha wilaya.
Swali: Je, vyumba vina kiyoyozi?
Hapana, vyumba havina kiyoyozi. Hata hivyo, kila chumba kina feni kwa kupoza hali ndani ya chumba. Eneo letu linanufaika na hali ya hewa tulivu, hivyo linahakikisha unapata starehe muda wote.
2. Booking na Malipo
Swali: Je, wageni wanaweza kufanya Booking mtandaoni au kupitia majukwaa ya mtandaoni (mfano, Booking.com)?
Booking mtandaoni bado haipatikani. Wageni wanaweza kufanya Booking kwa kututembelea, kutuma mtu au kwa kutupigia simu moja kwa moja.
Swali: Njia gani za malipo zinakubalika?
Tunakubali malipo kwa pesa taslimu, au uhamisho wa benki. Tunajitahidi kubadilika ili kukidhi mapendeleo yako.
Swali: Je, inahitajika kutoa malipo ya awali (amana) kwa ajili ya kufanya Booking?
Hapana, hatuhitaji malipo ya awali kwa ajili ya Booking.
3. Sera
Swali: Sera ya kusitisha makazi/mkataba ikoje?
Kughairi kuendelea kukaa kwetu ni rahisi—mjulishe tu msimamizi kuhusu nia yako.
Swali: Muda wa kuingia na kutoka ni upi?
- Kuingia: Kuanzia saa 5:00 asubuhi
- Kuondoka: Kabla ya saa 4:00 asubuhi
Swali: Je, wageni wanaruhusiwa kuleta wanyama?
Hapana, wanyama kama paka nk hawaruhusiwi.
4. Eneo na Upatikanaji
Swali: Nyumba ya wageni iko wapi?
Nyumba ya Wageni ya 'Sukuma Guest House' ipo takriban kilomita 100 kutoka katikati ya jiji la Mwanza katika mji wa Nyashimo, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu. Ipo kando ya barabara kuu ya Mwanza–Musoma na karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria.
Swali: Wageni wanawezaje kufika (usafiri wa umma, teksi)?
- Kwa gari binafsi
- Kwa usafiri wa umma: Mabasi yanayosafiri kutoka Mwanza kwenda Bunda, Bariadi, Musoma, Tarime, au Nairobi hupita mara kwa mara, takriban kila baada ya nusu saa.
Swali: Je, kuna vivutio karibu?
Ndio, kuna vivutio vya kusisimua karibu:
- Hifadhi Taifa ya Serengeti: Nyumba yetu ya kulala wageni ipo kilomita 40 tu kutoka Lamadi, ambapo kuna lango la kuingia hifadhini. Serengeti inajulikana kwa kuwa na makundi makubwa ya nyumbu, swala, na pundamilia, pamoja na uhamaji (migration) mkubwa wa wanyama na wa kipekee duniani. Ni Eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO na kivutio cha watalii wa kimataifa.
- Ziwa Victoria: Wageni wanaweza kufurahia uzoefu wa kitamaduni wa wenyeji, kama kutembelea vijiji vya wavuvi vilivyo karibu au kuagiza vyakula vya kiasili kwenye mgahawa wetu.
5. Huduma Maalum
Swali: Je, mnapokea wageni kutoka uwanja wa ndege au kuandaa ziara?
Hapana, kwa sasa hatupokei wageni kutoka uwanja wa ndege wala kuandaa ziara/safari za kitalii. Ila tunaweza kukuunganisha na wanaotoa huduma hizi Mwanza au Arusha.
Swali: Je, kuna mgahawa au jiko kwa wateja?
Ndio, Sukuma Guest House ina Pub/Bar na mgahawa wa ndani. Tunatoa:
- Aina mbalimbali za vinywaji
- Vyakula vitamu vya kimataifa, vya kiasili, ikiwemo vyakula vya Kisukuma
Chakula chote kinapikwa na Bi Shikalile, mmiliki wa Mgahawa wetu maarufu wa 'SHIKA Restaurant'. Mbali na malazi, tunawapa wageni fursa ya kufurahia ladha halisi za kiasili.